EMaS ni mfumo wa kisasa unaosaidia shule na halmashauri kusimamia mitihani, uingizaji wa alama, uchambuzi wa matokeo, na utoaji wa ripoti kwa usahihi na kwa wakati.
Kuwa mfumo unaoongoza Tanzania katika usimamizi wa mitihani kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye uwazi na ufanisi.
Kuwapa walimu na wasimamizi zana rahisi na salama za kuingiza alama, kuchakata matokeo, na kutoa ripoti kwa viwango bora.
EMaS imeundwa ili kutatua changamoto za muda mrefu katika uandaaji wa matokeo ya mitihani ya pamoja. Mfumo unarahisisha ugawaji wa majukumu (clerks/data entrants), huongeza uwazi katika uhakiki wa alama, na hutoa ripoti za kisasa kwa shule na halmashauri.
Tunazingatia matumizi rahisi, muonekano safi (UI), na utendaji wa haraka. EMaS inasaidia uendeshaji wa shule nyingi (multi-school), mitihani ya pamoja, rankings, na uchambuzi wa matokeo.
Unahitaji msaada, maelekezo, au unataka kuanza kutumia EMaS? Wasiliana nasi kupitia njia zifuatazo.
Jiunge na shule nyingi zinazotumia EMaS kuboresha uingizaji wa alama, uchambuzi wa matokeo, na usimamizi wa mitihani.